SHIGERU MINAMI

MADHARA YA UTAPELI YANAYOHUSIANA NA BITCOIN HIVI SASA NCHINI TANZANIA.

1.Utapeli wa Deepfake – Hasara ya Dola Milioni 1.48

🟣 Mwezi Februari 2025, akaunti ya X (zamani Twitter) ya bilionea wa Kitanzania Mohammed Dewji ilidukuliwa.

🟣 Wadukuzi walitumia video bandia (deepfake) kuhamasisha uwekezaji katika sarafu feki iitwayo $Tanzania Token, na kuwahadaa wafuasi zaidi ya milioni 2.2.

🟣 Ingawa Dewji alikanusha haraka na kupata tena akaunti yake, tayari watu walikuwa wamepoteza dola milioni 1.48.

2. Utapeli wa Mahusiano (Pig Butchering Scam)

🟣 Matapeli wanajifanya kuwa kwenye mahusiano ya mapenzi kupitia mitandao kama WhatsApp, Telegram au apps za kudate.

🟣 Wanajenga uaminifu na baadaye kumshawishi mhanga kuwekeza kwenye “fursa ya crypto” ambayo ni feki.

🟣 Aina hii ya utapeli imeenea sana hata Tanzania, japo si ya kipekee kwa taifa letu.

3. Kuongezeka kwa Visa vya Udanganyifu wa Crypto

🟣 Ripoti zinaonyesha ongezeko la asilimia 250 ya visa vya utapeli wa crypto nchini Tanzania katika nusu ya kwanza ya 2023.

🟣 Matapeli hutumia stakabadhi bandia na utambulisho wa kughushi kufanya udanganyifu kwa watu wasio na uelewa wa kina.

nostr:nprofile1qqs93ymetqpkem0f2ke9hy54swq5pw3dat9c6xfeakg6gxlz230xn9qpz4mhxue69uhk2er9dchxummnw3ezumrpdejqzrthwden5te0dehhxtnvdakqhxpm7s let me know if you need more...... you're welcome

Reply to this note

Please Login to reply.

Discussion

Asante sana kwa maelezo ya kina! Nitayatumia kama rejea.