*MAKOSA 7 YA KUEPUKA UNAPOUZA BIDHAA KWENYE WHATSAPP STATUS YAKO !!*

*Usifanye Hivi Kama unauza Bidhaa/huduma Zako WhatsApp Status*

....Kama Umekuwa ukipost bidhaa kwenye WhatsApp status yako kisha watu wakaishia Kuview Tu bila Kununua basi kuna uwezekano unafanya kosa mojawapo kati ya haya 7

1). Kupost Picha Tupu Bila CAPTIONS yoyote...

Ukweli ni kwamba kinachouza bidhaa kwenye maandishi sio picha ni Caption ya picha. Iandae Caption yako vizuri na weka Taarifa zote za muhimu usisahau kuweka BEI😂

2). Kuwaambia Watu Kuwa Una Mzigo wa KUTOSHA au Mzigo Upo wa Kutosha...

Kama mzigo Upo wa kutosha kwanini ninunue Leo na sio kesho au kesho kutwa?

Jaribu kuonesha umuhimu, Uthamani una uchache wa Bidhaa zako ili mteja afanye maamuzi ya hataka 😇

3). Kutokuweka Bei kwenye bidhaa yako...

Kutokuweka Bei kwenye bidhaa yako kunaibua maswali mengi sana kichwani kwa mteja. Usiogope kuweka Bei hata kama ni kubwa, wenye uwezo watanunua na usiyowahusu wataView na kupita hivi 😂😂

4). Kutengeneza TAIRI Kwenye WhatsApp status yako...

Na Hili ni tatizo sugu sana kwetu

...Ukweli ni huu Hapa...

Ukimpa binadamu chaguo nyingi kwa Wakati mmoja Ghafla huwa anapatwa na tatizo la kufanya maamuzi. Mpe sample ya Bidhaa zako kali, ukiwa mtu wa kuweka TAIRI mteja atakushusha chini (mute😂)

5). Hakuna bei pekee Bila Uthamani wa bidhaa.

Hii kitaalamu inaitwa—Price Anchoring”

Mfano...

Bidhaa Hii kwa Leo inauzwa Tshs 20K Tu lakini Thamani yake ni Tshs 50K

6. Unaweka picha au Video zisizo na ubora na Maadili.

…Mfano mtu anauza nguo anatupostia picha za kudownload za wazungu au wadada wapo uchi.

7. Huonekani mara kwa mara Online na hujibu Jumbe za watu kwa wakati.

WhatsApp status ni njia rahisi, Rafiki, salama kuuza na kununua Bidhaa.

Graysatoshi

Digitalpreneur

Reply to this note

Please Login to reply.

Discussion

No replies yet.