*Soma Kwanza Hii Kabla ya Kuandika Tangazo Lako...*
Kama unahitaji Kuandika Tangazo Lenye kukuleta Mvua ya Wateja mtandaoni somo mpaka mwisho
Kama unahitaji kugeuza Tangazo lako Kuwa kariakoo au mlimani City makala hii ni zaidi ya zawadi kwako
Kwanza kabla ya Kuandika Tangazo lako
Unatakiwa ujue kwamba Tangazo lako Ndio mtu wako wa Mauzo
Unapoandika Tangazo lako hakikisha unajua kinachotatuliwa na bidhaa/huduma yako
Ili Tangazo Lako Likuletee Matokeo hakikisha Lina vitu Vifuatavyo...
1). Tatizo la Mteja
Elezea tatizo Lao vizuri na kwa ufasaha zaidi Kuliko wao wenyewe
Elezea tatizo lake kiasi kwamba akisoma mpaka aseme “Wow, huyu kweli ananijua na kunielewa”
Wateja hununua vitu kwasababu wamehisi wameeleweka kwa muuzaji sio kwasababu wameielewa bidhaa yako
Watu hununua zaidi vitu ili kutoka kwenye maumivu Kuliko kuingia kwenye raha
2). Faida za Vipengele vya Bidhaa/huduma yako
Hakuna anaenunua gari kwasababu ya vyuma vilivyomo ndani, watu hununua kile kinachofanywa na gari kwao
Uza faida za vipengele vya bidhaa yako na sio vipengele Kama Jinsi vilivyo (kosa la wengi hili)
3). Kichwa cha Habari (Headline)
Ukitaka Tangazo lako lisomwe hakikisha lina headline, Matangazo mengi online hayana headlines kabisa
Kwanini Headline ni muhimu Zaidi Kuliko kitu chochote kwenye Tangazo lako?
Kwasababu 60% ya wateja husoma headline tu
Wateja husoma headline Mara tano zaidi ya wanavyosoma Tangazo zima
4). Jibu Vipingamizi vyao juu ya Kile unachokiuza
Tangazo zuri lazima liwe na majibu ya vipingamizi Vyote vya wateja Juu ya Bidhaa/huduma
5). Waambie Jinsi ya kupata kile unachokiuza (Call to Action/CTA)
Wengi hukosa mauzo kisa tu hawajawaambia wateja Jinsi ya kupata bidhaa/huduma zao
Waambie wafanyaje ili wapate Bidhaa au huduma yako mwisho wa Tangazo lako
Digitalpreneur