VITU VITATU MUHIMU KULIKO MUDA UNAOTUMIA KUPOST.
(1) Solve Problems
Je maudhui ambayo unapost yamelenga kukunufaisha wewe au mteja wako? Na je maudhui ambayo unapost yanashawishi mteja kuendelea kukutazama na kukufuatilia?
Ili kuandaa maudhui bora unapaswa kujua changamoto ambazo wateja au watu wanapitia kisha njoo na suluhisho sahihi ambalo ndio njia ya wewe kuuza bidhaa yako au huduma yako.
Watu hawataki bidhaa au huduma yako ila wananunua suluhisho la matatizo Yao.
2) Strong Hook
Baada ya kuwa na heading kali sana basi jambo linalofuata ni kuwa na hook ambayo hii kazi yake kubwa sana ni kuvuta attention ya mteja kutamani kufahamu nini unauza na kuwavutia kununua ili kuelewa hook vizuri lazima uwe umesoma Course ya Copywriting Skills ndio utakuwa mbobevu mzuri zaidi.
Kama utashindwa kuwapa attention wateja au wanaokufuatilia basi hutawapata ama hata hao ulio wapata ipo siku nao watakukimbia
Tumia muda mwingi kuandaa post yenye kuibua hisia za mteja kuliko kukimbilia kupost bila kuwa na attention au strong hook.
Hook ndio humfanya mteja aweze kusoma tangazo lako mpaka mwisho.
Mfano.
Kichwa cha tangazo.
NAMNA YA KUOA BILA KULIPA MAHALI.
HOOK
Nitakupa njia tano zilizonisaidia kuoa bila mahari ila njia ya tano ndio niliyoipenda zaidi.
Mana hapo kisaikolojia kila mtu atatamani kuijua zaidi hiyo ya tano ina nini kumbe ndo ameshausoma ujumbe wako wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Hapo nimekupa tu mfano uone namna hook inaibua hisia kwa mteja kutaka kujua zaidi na zipo aina nyingi au mitindo mingi ya kuandika Hook.
3) KEYWORDS
Hapa unapaswa kuwa na maneno ambayo wateja hupenda kuyatumia pindi Wanapo tafuta bidhaa au huduma.
Kikawaida hata wewe kuna namna ukiwa unatafuta bidhaa au huduma fulani ukienda Instagram kuna namna una search majina ambayo unatarajia yatakusaidia wewe kupata wateja.
Mfano ukihitaji Umbea lazima vyovyote utakavyo andika ila utasearch maudaku au mastory hata page maarufu za udaku zinaandikwa fredmaudaku au carrymastory hujawahi kujua kwanini?
Sababu anakupa wepesi wa yeye kumpata hata kama ulikuwa hujamfollow.
Je Umejifunza kitu?