*Vitu Vya kuzingatia wakati Unauza Bidhaa/ huduma...*

*Fahamu hivi wakati wa kuuza.*

1). Attention hufuata Attention, Sehemu ulipoweka umakini wako ndipo mteja wako pia atapoweka umakini wake

Ukiweka umakini kwake nayeye ataweka umakini kwako, ukiweka umakini kwenye Bidhaa/huduma yako, nayeye ataweka umakini kwenye hela yake

2). Overselling ndio adui mkubwa zaidi wa mauzo yako

Wateja hawataki kusikia zaidi ya vile wanavyotaka kuvisikia na wala hawajali chochote kuhusu wewe

Mteja akiuliza muda mtajie muda, hahitaji kujua jinsi ya kutengeneza saa

3). Usiwauzie Unachotaka kuuza, wauzie wanachotaka kununua

Wateja hawapendi Kuuziwa ila wanapenda kununua

4). Ni ngumu sana kuuza Bidhaa/huduma kwa mtu asiekujua

Kwenye mauzo huwa sio unamjua nani Bali ni nani anakujua wewe

5). Unachohitaji kukijua zaidi ni Watu kuliko kile unachokiuza aidha ni Bidhaa/huduma

Upo kwenye biashara ya watu sio Bidhaa/huduma

6). Usipompitisha mteja katika hatua kuu 3, tegemea kukutana na kipingamizi mwishoni

Ambazo ni Agenda step, Qualify step na Commitment step, usiruke hata moja zipo page # 41 kwenye kitabu cha H.E.L.A

7). Usiwauzie Wateja wako Bidhaa/huduma Bali wasaidie kununua

Ndio maana ni vigumu kuuza kama hujui maumivu ya mteja

8). Uhitaji kuwa mwongeaji sana ndio uwe muuzaji mzuri, unachohitaji ni kuwa muuliza maswali na msikilizaji mzuri

Ukifanya hivyo Wateja watakwambia wanataka kununua kitu gani na wanataka kuuziwaje

9). Anaenunuliwa ni muuzaji sio Bidhaa/huduma kwasababu 90% ya mauzo yanatokana na Sauti + Ishara za mwili na 10% tu yanatokana na maneno

10). Selling na Closing ni vitu viwili tofauti na havifanyiki kwa wakati mmoja

Unapofanya Selling unatakiwa uache kufanya closing na unapofanya closing unatakiwa uache kufanya selling nje na hapo unakosa vyote

11). Kifaa muhimu kuliko vyote kwenye mauzo ni Masikio sio mdomo

Wauzaji wazuri ni wasikilizaji wazuri sio waongeaji wazuri

Devan

Digitalpreneur__

Reply to this note

Please Login to reply.

Discussion

No replies yet.