🟠 ADAM BACK: “100,000 ni bei ndogo sana, nategemea Bitcoin itamaliza mwaka kwa bei kubwa zaidi. Tunaweza kufika kati ya500,000 hadi 1M kwenye huu mzunguko.”

Adam Back, mwanzilishi wa kampuni ya teknolojia ya Bitcoin – Blockstream, na mmoja wa watu waliotajwa katika whitepaper ya Bitcoin na Satoshi Nakamoto, anaamini kuwa thamani halisi ya Bitcoin bado haijafikiwa.

Kauli yake inaonyesha matumaini makubwa kuhusu mwenendo wa soko la Bitcoin katika kipindi hiki cha mzunguko wa soko (market cycle). Anaona kuwa kiwango cha100,000 kwa Bitcoin si kikubwa kama wengi wanavyodhani, bali ni bei ndogo ukilinganisha na uwezo halisi wa Bitcoin kama hifadhi ya thamani (store of value) inayojitegemea na isiyodhibitiwa na serikali yoyote.

Kulingana naye, nguvu ya soko, mahitaji kutoka kwa wawekezaji wakubwa, mashirika, na hata mataifa, inaweza kuisukuma Bitcoin hadi bei ya nusu milioni hadi milioni moja kwa kipande kimoja.

Hii ni ishara kwa watu kuzingatia uwekezaji wa mapema, kwani mabadiliko makubwa ya thamani yanaweza kutokea kwa kasi.

#Bitcoin #AdamBack #BTC500K #BTC1M #Hyperbitcoinization #DigitalGold #BitcoinCycle #StoreOfValue #CryptoFuture #BitcoinAfrica #BitcoinTanzania

https://blossom.primal.net/b66b9bb1a4f00d87e453dbb38950e95d866f8b5107e7e69b564b2feca061e338.mp4

Reply to this note

Please Login to reply.

Discussion

No replies yet.