Kwa Mfanyabiashara...!

...Ijue Mbinu Hii unayofanya Kazi Zaidi Ya 80% Kwenye Mauzo

Mteja akija kwako akaulizia kitu na kukikosa, usiishie kumuambia kwaheri. Muombe namba ya simu, muambie kikija utamtarifu. Au mpe muda fulani, mfano, wiki ijayo utakuletea mzigo mpya karibu...

...Ukishajichukua namba yake ya simu hakikisha kuwa unaisave na anaisave yako...Utajuaje? Mtajie kwanza yako, kisha muombe akubeep. Halafu mtajie jina lako la kusave.

Au akishakutaji mbeep kisha muambie jina lako, yaani kuwa kama unamuangalia ilia save namba yako!

Muambie asave namba kwa biashara yako, kwa mfano, unaitwa Juma unauza Mashati, basi muambie asave “Juma Mashati Kariakoo”...Siku nyingine akiwa na shida ya shati ni rahisi kukukumbuka kuliko kuandika ‘Juma’ tu!

Hata kama siku hiyo hatanunua, hata kama hatarudi tena, lakini kwa kuwa na namba yako moja kwa moja inamaanisha ataona status zako na kujua bidhaa nyingine ambazo unazo.

Digitapreneur

Complex Into Simple

Devan

Reply to this note

Please Login to reply.

Discussion

No replies yet.