📢 HABARI NJEMA MPYA!

JacK Dorsey kupitia mradi wake wa bitchat ameonesha video mpya inayoonesha jinsi mfumo wa kutuma ujumbe unavyofanya kazi kwa kutumia Bluetooth tu bila intaneti kabisa.

Hii ni teknolojia ya kipekee ambayo inaruhusu watumiaji wa Bitcoin kuwasiliana kwa usalama, kasi na uhuru hata katika maeneo ambayo hakuna mtandao wa intaneti.

Kwa kutumia bitchat , ujumbe wote unatumwa kwa njia ya usimbaji fiche (encrypted), hivyo hakuna mtu wa tatu anaweza kusoma au kufuatilia mawasiliano yako. Hii inaleta mapinduzi makubwa katika usalama wa mawasiliano, hususani kwa watu wanaoishi maeneo ya vijijini au kwenye maeneo yenye changamoto za mitandao.

Mfumo huu unaendana na falsafa ya Bitcoin – kuleta uhuru wa kifedha na mawasiliano bila kutegemea mifumo ya kati (centralized systems) .

bitchat ni suluhisho bora kwa wa-Afrika na dunia nzima, ikitoa njia mbadala, salama, na ya kuaminika ya kuwasiliana popote ulipo.

🙌 Tunamshukuru Jack Dorsey kwa ubunifu huu mkubwa unaoimarisha uhuru wa kidijitali.

Kwa wale wanaotamani kujaribu nenda appstore au playstore pakua app inaitwa Bitchat na uwone inavyofanya kazi .

#BitChat #Bitcoin #BluetoothMessaging #NoInternet #JackDorsey #Africa #DigitalFreedom #BitcoinSafariTz #TanzaniaBitcoin

Reply to this note

Please Login to reply.

Discussion

No replies yet.