FAHAMU KWA HARAKA: DeFi NI NINI?
Leo tujifunze DeFi (Decentralized Finance) - hii ni moja ya nguzo muhimu sana kwenye crypto na blockchain.
DeFi ni nini?
DeFi ni kifupi cha Decentralized Finance, yaani huduma za kifedha zisizo na benki au mtu wa kati, zinazoendeshwa na blockchain, hasa Ethereum.
Kwa lugha nyepesi: DeFi ni benki ya mtandaoni isiyo na benki,
π Hakuna manager, hakuna karani, hakuna makaratasi,
π Wewe na blockchain mnafanya miamala moja kwa moja.
Kupitia DeFi unaweza:
1.Kukopesha pesa (crypto)
2.Kukopa pesa
3.Kupata riba
4.Kufanya trading
5.Kuweka akiba
6.Kununua insurance
7.Kuweka bets (long & short)
Yote haya bila benki.
Kwa nini DeFi ni muhimu?π
Bitcoin ilianza kama pesa ya kidigitali
DeFi ikaenda mbali zaidi:
π Ikajenga mfumo mzima wa kifedha mbadala wa Wall Street,
π Bila majengo makubwa,
π Bila mishahara ya mabenki,
π Bila vikwazo vya nani aruhusiwe au asiruhusiwe.
Mtu yeyote mwenye Simu, Internet,Wallet anaweza kushiriki DeFi
Hii ina maana kuwa:
- Fursa sawa kwa wote
- Hakuna kubaguliwa
- Hakuna kuulizwa βunafanya kazi gani?β
Faida za DeFi
_1. Iko wazi kwa wote_
Huhitaji kufungua akaunti benki. Unatengeneza wallet tu kama MetaMask then unaanza.
_2. Hakuna taarifa binafsi_
Hakuna jina
Hakuna email
Hakuna NIDA
Hakuna KYC
Wallet yako ndio utambulisho wako.
_3. Uhuru kamili_
Unaweza kutuma pesa muda wowote
Hakuna kuomba ruhusa
Hakuna kusubiri siku 3-5
Hakuna ada kubwa za kibenki
5. _iko chapu sana_
Riba hubadilika kila sekunde chache (kama sekunde 15)
Mara nyingi riba ni kubwa kuliko benki za kawaida
_6.Transparent_
Miamala yote iko wazi kwenye blockchain
Kila mtu anaweza kuona kilichofanyika
Hakuna kuficha hesabu kama kampuni binafsi
DeFi inafanyaje kazi?
Badala ya benki, DeFi hutumia DApps (Decentralized Applications).
DApps ni apps zinazotengenezwa juu ya blockchain hasa Ethereum
Mfano
Unafungua DApp
Unaconnect wallet yako
Unaanza kutumia huduma
Hakuna fomu, Interview wala Approval ya mtu
Matumizi ya DeFi kwa sasa
1. Kukopesha
Unakopesha crypto yako,
Unapata riba kila dakika, sio mwisho wa mwezi.
2. Kukopa pesa
Unakopa papo hapo
Hakuna makaratasi
Kuna hadi flash loans (mikopo ya sekunde chache)
Benki za kawaida haziwezi hili.
3. Trading
Unanunua na kuuza crypto moja kwa moja
Hakuna broker
Hakuna middleman
Ni kama trading ya hisa bila broker.
4. Akiba
Unaweka crypto kwenye platforms za DeFi, Unapata riba nzuri kuliko benki nyingi.
5. Derivatives (Long & Short)
Unabet bei ipande (long)
Unabet bei ishuke (short)
Ni kama options au futures kwenye soko la kawaida.
Hasara na hatari za DeFi
Tusifundishe DeFi bila kuongelea hatari
1. Ada za mtandao (Gas fees)
Ethereum chain ikizidi kuwa busy, ada inapanda
Hivyo ku trade mara nyingi inaweza kuwa ghali
2. Volatility
Bei hubadilika haraka
Unaweza kupata faida au hasara kubwa
3. Kodi na sheria
Hakuna mtu anayekufanyia hesabu za kodi
Wewe mwenyewe unatakiwa kufuatilia
Sheria zinatofautiana nchi hadi nchi
Hitimisho
DeFi ni: - Mfumo wa kifedha wa kizazi kipya
- Usio na benki
- Wazi kwa wote
Lakini una hatari zake
π Elimu ni muhimu kabla ya kutumia DeFi.
