Habari Mpya kwenye Crypto Adoption - Marekani
_Nini kimetokea?_
Tarehe 20 Desemba 2025, wabunge wa Marekani kutoka pande zote mbili za siasa
Rep. Max Miller ws Republican - Ohio na
Rep. Steven Horsford wa Democrat - Nevada
walitoa rasimu ya majadiliano yani discussion draft ya sheria mpya inayoitwa Digital Asset PARITY Act.
Sheria hii inalenga mfumo wa kodi (tax framework) kwa crypto, hasa stablecoins.
Kipengele kikubwa zaidi (SAFE HARBOR)
Sheria inapendekeza kutokutoza capital gains tax kwa:
Malipo yanayotumia stablecoins zilizofungamana na dola ya Marekani ikiwa thamani ya muamala ni chini ya USD 200.
👉 Hii inalenga matumizi ya kila siku, kama:
- Kulipa huduma
- Kununua bidhaa ndogo
- Kutuma pesa ndogo
Lengo ni kupunguza usumbufu wa kodi (IRS compliance burden) kwa wananchi wa kawaida.
_Masharti ya stablecoin zinazokubalika_
Ili stablecoin ifaidike na msamaha huu:
Iwe imetolewa na issuer aliyeidhinishwa chini ya GENIUS Act
Iwe imefungamana moja kwa moja na dola ya Marekani pekee
Bei yake ibaki ndani ya 1% ya $1 kwa angalau 95% ya siku za biashara kwa mwaka uliopita
👉 Sio stablecoin zote, ni zile zilizokuwa regulated kikamilifu.
_Nani hawahusiki?_
Msamaha huu hauwahusu
- Brokers
- Dealers
- Trading au investment activities
👉 Hii si sheria ya kuwakinga traders wakubwa,
👉 Ni kwa matumizi madogo ya kila siku, si faida kubwa za uwekezaji.
_Kitu kinachoendelea kujadiliwa_
Wabunge bado wanajadili:
Kuweka kikomo cha jumla cha mwaka (annual aggregate cap)
ili kuzuia watu kutumia loophole.
_Itaanza lini?_
Kama sheria hii itapitishwa:
Itaanza kutumika kwa miaka ya kodi baada ya Desemba 31, 2025
_Hali ya sasa_
Hii ni rasimu tu, bado sio sheria rasmi
Bado haijawasilishwa rasmi bungeni
Lakini ni pendekezo la kwanza kabisa la kodi ya crypto
kutoka kwa wajumbe wa House Ways and Means Committee.
Hii ni ishara kubwa kwamba:
Serikali ya Marekani imeanza kuichukulia crypto kama sehemu ya mfumo wa fedha,stablecoins zinaonekana kama njia halali ya malipo ya kila siku
_Hitimisho_
Hii si habari ndogo.
Ni hatua ya wazi kuelekea:
Crypto kutumika kama pesa za kawaida
Stablecoins kuwa daraja kati ya crypto na mfumo wa fedha wa kawaida
